Mkurugenzi
Wa Mafunzo Taifa Benson Kigaila akielezea tukio lilivyokuwa kwa
waandishi wa habari leo.
---
Na Francis Godwin, Iringa.
Ikiwa
ni siku tano zimepita toka kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa channel
ten na mwenyekitiwa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi mwangosi
katika vurugu baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo mafinga.
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kupitia viongozi wake Iringa
wameongea na waandishi wa habari kuhusu kile kilichotokea.
Akiongea
na waandishi wa habari Iringa leo Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni
ya Movement For Change Taifa Benson kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa
la Chadema tarehe 2.09.2012 kule Nyororo walikuwa na lengo la kufungua
matawi na kufanya vikao vya ndani na wanachama wao na sio kufanya
mikutano ya hadhara kama inavyosemekana.
Aliendelea
kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa tawi katika ofis ya kata
Nyororo Polisi wafika na kutangaza kuwa watawanyike na wakamueleza RCO
kuwa wapo kwaajili ya kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani na kwamba
polisi wakiingilia ndio watakao kuwa wanachochea vurugu.
Aidha
Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo wakifungua Tawi hilo vyama
vingine kama CCM nchi nzima walikuwa wakifanya chaguzi katika ngazi za
Wilaya lakini hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni kuingilia zoezi la
sensa.
Baada
ya kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa wanaelekea ofisi ya kata
ili wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC Kamuhanda ndipo
alipoagiza na kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha watu na
kufunga mkutano” alisema Kigaila.
Wakati
wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu mwangosi alimueleza kigaila
kuwa anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa polisi wanaonekana si wa
Iringa jambo ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuuwawa kwake.
Huku akihoji kuhusu kamera na laptop za marehemu kutoonekana na
kutotolewa taarifa mpaka sasa.
Naye
katibu mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea maneno ya mwisho ya
marehemu alisema kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa wamwachie kwani
yeye yuko kazini wasimuue kwani anatekeleza majukumu yake “ Jambo ambalo
polisi hao hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga mpaka umauti
ulipomfika.
Aidha
Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi walikuwa katika tukio hilo wako
tayari kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa na si Tume
iliyoundwa na Jeshi la polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa macho yao
waliona polisi ambao wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana
hiyo.
Katibu
wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Deogratias Munishi ameeleza
“Kuhusu kauli ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa haina maana kwani
alitegemea yeye kama mlezi wa vyama vya siasa angefika katika eneo la
tukio ili aweze kuwa na ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye
vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao kama vyama vya siasa”
No comments:
Post a Comment