Mwandaaji wa shindano hilo atipokua akizungumza na waandishi wa habari.
Warembo
wanaoshiriki kwenye shindano la Redds Miss Ilala wakiwa kwenye picha
ya pamoja tayari kabisa kuingia kwenye fainali itakayofanyika jumamosi
hii kwenye ukumbi wa Nyumbani Kinondoni namanga jijini Dar es salaam.
WASANII
nguli wa miondoko ya bongofleva sanjari na Machozi Band, kesho
watalipamba shindano la kumsaka mrithi wa Salha Israel katika shindano
la Miss Ilala litakalofanyika kwenye ukumbi wa nje wa Nyumbani Lounge
uliopo maeneo ya Namanga, Dar es Salaam.
Wasanii
hao ambao watatumia bendi katika kuonesha umahiri wao, wamejumuika
kwenye shindano hilo ili kukidhi kile mashabiki wa Miss Ilala
wanachotarajia. Mbali ya wasanii hao, msanii wa luninga, Steve Nyerere
ndiye atakayeliongoza kama MC ambapo Alhamis(kesho) watakuwa na mkutano
na waandishi wa habari kwenye club ya City Sports Lounge kwa ajili ya
kutangaza zawadi.
Vimwana
14 wanaotarajiwa kupanda jukwaani kuwania umalkia wa Kanda ya Manispaa
ya Ilala, Redds Miss Ilala 2012, kati yao 12 wiki iliyopita walishindana
kwenye kategoria ya kipaji ambapo watano kati yao walitinga hatua ya
fainali, ambayo itamaliziwa siku ya shindano lenyewe Ijumaa.
Katika
kinyanganyiro hicho mrembo Mary Chizi alikuwa kivutio zaidi kwa jinsi
alivyoonesha umahiri wake wa wepesi wa kujvingirisha mwili huku Mectilda
Martin akizoa ukumbi mzima kwa kurap na huku akiwa ameandana kwa
kucheza hata mavazi yanayotumiwa na wasanii wa miondoko hiyo.
Magdalena
Munisi hakuwa nyuma kabisa katika kumwigiza mwanamuziki nguli wa
marekani, Ciara kwa umahiri wake wa kulitumia jukwaa, lakini kubwa
kuliko pia kwa mrembo Amina Sangawe alibuni nguo kwa kutumia vipande
viwili vya khanga ambapo aliliunganisha jukwaani kupitia pini nakumvika
mmrembo mwenzie. Stella Moris kwa upande wake alionesha ukali kwa
kuimba.
Warembo
hao, wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi,
Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss
Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na Dickson Daudi wa THT katika shoo.
Miss
Ilala, yenye rekodi ya kutoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss
Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe
aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na Salha Israel anayeshikilia
taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake nzuri mwaka huu.
Miss
Ilala inahusisha warembo kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata
na Ukonga na inadhaminiwa na City Sports Lounge, Redd's Premmium Cold,
Uhuru One, Dodoma Wine, Nyumbani Lounge, gazeti la Jambo Leo, 100.5
Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM.
Mbali
ya walioingia tano bora katika vipaji, warembo wengine wanaoshiriki
shindano hilo ni pamoja na Mary Chizi, Matilda Martin, Magdalena Munisi,
Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris na Elizaberth Pertty.
Wengine ni Wilmina Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon,
Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.
Mbali
ya Redd's Premmiun Cold, wadhamini wengine katika mashindano hayo ni
pamoja na Uhuru One, Dodoma Wine, City Sports Lounge, gazeti la Jambo
Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM na
Amaya Salon.
No comments:
Post a Comment