Asilimia
tano ya mapato yatakayopatikana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii
(Community Shield) kati ya Simba na Azam yatakwenda kwenye Hospitali ya
Temeke mkoani Dar es Salaam.
Kabla
ya kukabidhi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakutana
na uongozi wa Hospitali ya Temeke kupanga maeneo ambayo fedha hizo
zitatumika kwenye hospitali hiyo.
Mechi
hiyo ya uzinduzi rasmi wa msimu wa 2012/2013 itafanyika Jumanne ya
Septemba 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa
10 kamili jioni.
Viingilio
kwenye mchezo huo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na
kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa viti vya
VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
WACHEZAJI WAWILI WAOMBEWA ITC URENO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu la Ureno (FPF) limetuma maombi Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kupatia Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa
wachezaji wawili waliokuwa wakicheza mpira nchini.
Wachezaji
wanaoombewa ITC ni Hamis Thabit Mohamed (19) ambaye klabu yake ya
mwisho aliyoichezea nchini ilikuwa African Lyon wakati mwingine ni Abuu
Ubwa Zuberi (20) ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea timu ya
Yanga.
Kwa
mujibu wa FPF, wote wawili wanaoombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa
(amateur) ili waweze kujiunga na timu ya Atletico Sport Clube ya Ureno
ambayo hata hivyo haikuelezwa iko daraja gani nchini humo.
Pia
FPF imeombwa kupatiwa hati ya maelezo ya mchezaji (player’s passport)
kwa kila mmoja ikiwemo taarifa za ushiriki wao katika mechi rasmi
zinazotambuliwa na TFF wakiwa katika klabu zao hizo za zamani.
No comments:
Post a Comment