“Matumaini
yangu ni kwamba nitakuwa hapa kwa muda mrefu. Hii ni klabu kubwa na
acha niwe mwaminifu, hivi unaweza kutamani kutoka katika klabu kama hii?
Imekuwa ni timu kubwa duniani”
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney juzi usiku
amevunja ukimya na kuimbia klabu yake ya Manchester United kuwa yeye
anatarajia kukaa kwa muda mrefu klabu Old Trafford, kama anavyotaka
mwenyewe.
Rooney nyota wa kimataifa wa England,
amekuwa na mwanzo mbaya wa msimu klabuni hapo na kuzua maswali, ikidaiwa
kuwa ana mahusiano mabaya na bosi wake Mskochi Sir Alex Ferguson.
Mkali huyo kwa sasa anaguguza jeraha la
kuchanika juu ya goti lake kutokana na kuchimbwa na daruga la nyota wa
Fulham Hugo Rodallega na yuko nje ya dimba kwa miezi miwili, akitakiwa
kurejea kupigania namba pindi atakapopona.
Lakini juzi usiku Rooney, 26, akasema
anajisikia furaha kuwa sehemu ya kikosi chake na kwamba anakusudia
kuhitimisha zama zake dimbani akiwa na United, akisisitiza kuwa analeta
kuwa na muongo mmoja wa aina yake akiwa na Mashetani Wekundu hao.
Shujaa huyo wa zamani wa klabu ya Everton,
alisema: “Naweza kuwa hapa kwa miaka mingine 10? Natumaini itakuwa
hivyo. Kama nilivyopania kwa muda mrefu kuwa hapa, kisha na nikawa
hatimaye mchezaji wa Manchester United.
“Ni wazi kwamba nilikumbana na hali ngumu
hapa miaka michache iliyopita, lakini nikaweka wazi haraka sana kuwa
nilifanya makosa. Kama muda mrefu watu wanavyotaka mimi kuwa mchezaji wa
United, basio ndivyo nitakavyokuwa.
“Matumaini yangu ni kwamba nitakuwa hapa
kwa muda mrefu. Hii ni klabu kubwa na acha niwe mwaminifu, hivi unaweza
kutamani kutoka katika klabu kama hii? Imekuwa ni timu kubwa duniani,”
alisisitiza Rooney.
Rooney akaongeza kuwa anahitaji kuangalia
kila pande ya chumba cha kuvalia cha klabu yake ya kuona ni namna gani
anaweza kuboresha kazi akiwa na United kwa muda mrefu kadri
iwezekanavyo.
Akasema: “Unapaswa tu kuwaangalia nyota
kama Ryan Giggs na Paul Scholes na namna walivyopata mafanikio, wao ni
mfano wa kuigwa nasi sote. Hilo ndilo wazo na mpango wangu na nina
matumaini itakuwa hivyo pia,” alimaliza Rooney
No comments:
Post a Comment