Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 2, 2013

BLAD KEY AJIPANGA KIVINGINENa Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Awadhi ‘Blad Key’, amewataka wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya burudani ambazo amewaandalia na kwamba anakuja na staili mpya.
Licha ya kuwa na vibao vingi, Blad Key alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Vimepanda Bei’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri katika soko la muziki huo.
Akizungumza Dar es Salaam, Blad Key alisema ana nyimbo tatu ambazo tayari amezitengeneza na yuko katika mchakato wa kuchagua ipi itangulie na ipi ifuate.
“Nimetengeneza nyimbo tatu kwa mpigo zenye ujumbe tofauti, sijajua ni ipi itangulie kutoka na bado sijazipatia majina; nafikiri wiki ijayo nitakuwa nishazitafutia majina,” alisema Abdukiba.
Aliwaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuzipokea kazi hizo, ambazo ana uhakika zitafanya vizuri kutokana na ujumbe ulioko ndani yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...