Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 3, 2013

SHILOLE, MASANJA DAY 3 WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC


Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka (kati) akiwakaribisha Masanja na Shilole wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani, Bwn. Baraka Daudi (kushoto) na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ya maandalizi Bwn. Idd Sandaly Ubalozini hapo Jumanne July 2, 2013 walipokwenda kumtembelea na kufanya kikao kwa kumuelezea Kaimu Balozi maandalizi ya sherehe hii itakayofanyika Jumamosi July 6, 2013 yalikofikia.
Masanja akitia saini kitabu cha wageni Ubalozini hapo.
Shilole akitia saini kitabu cha wageni Ubalozini hapo.
Kutoka kushoto ni Baraka Daudi, Kaimu Balozi mama Lily Munanka, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly, Shilole na Masanja Mkandamizaji wakiongea jambo walipokua Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Masanja na Shilole katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
Kamati ya Maandalizi wakitoa taarifa kwa Kaimu Balozi mama Lily Munanka maandalizi yalikofikia.
Nyammy katika picha ya pamoja na Shilole na Masanja.
Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na Mariam.
Mama Love Maganga akipiga picha ya pamoja na Masanja na Shilole.
Shilole na Masanja walipotembelea ofisi za Community Mult Services, Inc zilizopo Silver Spring, Maryland.
Kutoka kushoto ni Mr. Watson, Ms Patricia, Jamila, Shira, Mrs Reese, Shilole, Masanja na Baraka katika picha ya pamoja.
Masanja na shilole wakipata Dinner ya mchana kwenye mgahawa wa Kijiji cha Swahili.
 Mussa Shedafa katika picha ya pamoja na wasanii

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...