Picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya jiji la
Mwanza.
Sehemu ya vyandarua vilivyotolewa msaada vikiwa tayari
vimefungwa na wasanii wa filamu hapa nchini,mara baada ya kutoa msaada wa
vyandarua hivyo ndani ya wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Mkoa wa jiji la
Mwanza-Sekou-toure mapema leo
asubuhi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WASANII maarufu wa Bongo Movie hapa nchini, ambao wapo hapa kwa
ajili ya Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania
Open Film Festival’ jana walikabidhi vyandarua kwa Halmashauri ya Jiji la
Mwanza pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure.
Akizungumza na wasanii hao, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa
Hassan Hida, aliwashukuru wasanii hao kwa msaada huo na kuwataka wawasaidie pia
wasanii wachanga wa jijini hapa ili nao waweze kutoka.
“Nimefarijika na msaada huu pamoja na ujio wenu, ila kimoja
ninachokiomba kutoka kwenu ni kuwasaidia wasanii wa Mwanza ili nao waweze
kutoka, naamini ujio wenu ni changamoto kubwa kwao,” alisema Hida.
Kaimu Meya wa Jiji la Mwanza, Dismas Masuni naye alitoa shukrani
kwa msaada huo na kusema wapo ni vema zaidi kwa wasanii hao pia kufikiria
kuwekeza jijini hapa kwa ajili ya maendeleo yao.
Meneja wa kinyawaji cha Grand Malt, Consolata Adam, alisema nia
kubwa ya kuamua kudhamini tamasha hilo ni kuwaendeleza zaidi vijana kwani wengi
wako katika ajira hiyo na kutaka wakazi wa Mwanza kufika kwa wingi wakati wote
wa tamasha hilo.
Wakati walipokabidhi msaada wa vyandarua katika hospitali ya
rufaa ya Sekou Toure na kuvifunga katika wadi ya wazazi, wasanii hao
walionekana kuguswa zaidi na hali ilivyo na kusema wana jukumu kubwa la
kuisaidia jamii. Katibu wa Afya wa hospitali hiyo, aliye pia kaimu Katibu wa
Afya wa Mkoa, Danny Temba alishukuru kwa msaada huo na kusema umekuja wakati
muafaka kutokana na mahitaji yaliyopo.
“Tunashukuru mno kwa msaada wenu na kwa kutaka kuwadhihirishia
tuna mahitaji makubwa na vyandarua hasa katika kupambana na malaria, naomba
mkavifunge wenyewe,” alisema Temba, ombi lililoridhiwa na wasanii hao na kuomba
wavifunge katika wadi ya mzazi na mtoto.
Wasanii walionekana kuguswa zaidi walipoingia katika wadi hiyo,
huku Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Chuchu Hans, Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi
‘Ray’, Hashim Kambi na wengineo wakionekana kuguswa zaidi na mahitaji ya wadi
hiyo.
“Kuna mahitaji makubwa katika hospitali hii, kuna kitu
kimenigusa mno kwa kuja hapa,” alisema Jacob Steven ‘JB’, huku akiungwa mkono
na Single Mtambalike ‘Ritchie Ritchie’ na Steve Nyerere.
Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, ambalo lilizinduliwa
rasmi jana katika Uwanja wa Nyamagana alisema, kutakuwa na filamu za aina
mbalimbali zitakazoonyeshwa wakati wote wa tamasha hilo.
Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu
wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake na
kuwataka wakazi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kushuhudia mambo yanayoendelea.
Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani
wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. “Tumejipanga katika
hili na wala hatutanii. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu
za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa
zaidi,” alisema Consolata.
Tamasha
hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi
ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Msanii wa Bongo Movie,Jacline
Wolper akiwa katika wodi ya wazazi ,Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekou-toure
akifunga chandarua kwenye moja ya vitanda hospitalini hapo,ikiwa ni sehemu ya
vyandarua vilivyotolewa na wasanii hao kupitia kinywaji cha
Grandmalt
Wasanii Irine Uwoya na Shamsa
Ford wakiwa na mmoja wazazi akiwa amembeba mtoto aliezaliwa kwenye hospitali
hiyo ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure mara baada ya wasanii hao
kutembelea Hospitali hiyo na kutoa vyandarua kwenye wodi
Wazazi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Halifa
Hassan Hida akizungumza machache (mbele ya wasanii wa Bongo Movie (hawapo
pichani) ikiwemo na kuwashukuru wasanii hao wa filamu kwa kitendo cha kiungwana
kabisa katika suala zima la kuisaidia jamii yao inayowazunguka kwa njia moja ama
nyingine na pia amewataka kuwasaidia wasanii wachanga wa jiji la Mwanza na
kuwaelekeza njia sahihi za mafanikio katika tasnia hiyo ambayo kwa sasa imezidi
kushika kasi siku siku.
Meneja wa kinywaji cha Grandmalt
Consolata Adam akipokea mkono wa shukurani kutoka kwa katibu wa Afya hospitali
ya Sekou-toure
Bwa.Daniel Temba,mara baada ya kabidhi msaada wa vyandarua
sanjari na wasanii mbalimbali wa filamu,makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo
kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure,ikiwa ni sehemu ya wasanii hao
kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Wasanii mbalimbali wakiongozwa na
Raymond Kigosi wakikabidhi msaada wa vyandarua
kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure, kwa katibu wa afya wa Hospitali
hiyo Bwa.Daniel Temba ikiwa ni sehemu ya wasanii hao
kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
wasanii wakiendelea na zoezi
la wakikabidhi msaada wa vyandarua
kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure kwa katibu wa afya wa
Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya wasanii
hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Baadhi ya wasanii wa Filamu hapa nchini a.k.a Bongo
Movie Unity wakiwasili kwenye hospitali ya Sekou-toure tayari kwa kushiriki
zoezi la kugawa vyandarua kwenye wodi ya wazazi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji
kisicho na kilevi cha GrandMalt mapema leo
asubuhi.
Mlezi wa Bongo Movie Unity,Jacob Steven a.k.a JB a.k.a
Bonge la Bwana wakisalimiana na Afisa mhausiano wa Halmashauri ya jiji la
Mwanza,Bwa.Joseph Mlinzi,pichani kati ni msanii wa filamu Singo
Mtambalike.
Baadhi ya Wasanii hao wa Bongo Movie Unit wakitoka
kwenye wodi ya Wazazi mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua vilivyotolewa
kwa hisani kubwa ya kinywaji kisicho na kilevi cha
Grandmalt.
No comments:
Post a Comment