Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 3, 2013

Kundi la ngoma za asili la Ruau limefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya ngoma mkoa wa Kagera chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha BALIMI EXTRA LAGER.


 Baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera ambao walijitokeza kwa wingi katika viwanja vya kaitaba kushuhudia fainali za Ngoma za Asili kwa Mkoa huo ambyo mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
 Wasanii wakiwa kazini katika fainali za Ngoma za Asili kwa Mkoa huo ambyo mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Pangani  akimkabidhi kiongozi wa kundi la Ruau Bw Ezekhiah Henriko kitita cha shilingi laki 6 ikiwa zawadi ya mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano Ngoma za Asili kwa Mkoa wa Kagera, katikati ni Afisa utamaduni Manispaa ya Bukoba Evarisia Ruafiyami na Meneja masoko Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Bw Andrwe Mmbwambo,Mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Pangani  akimkabidhi kiongozi wa kundi la Ruau Bw Ezekhiah Henriko kitita cha shilingi laki 6 ikiwa zawadi ya mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano Ngoma za Asili kwa Mkoa wa Kagera, katikati ni Afisa utamaduni Manispaa ya Bukoba Evarisia Ruafiyami na Meneja masoko Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Bw Andrwe Mmbwambo,Mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
Kundi la ngoma za asili la Ruau limefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya ngoma mkoa wa Kagera chini ya udhamini wa  
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha BALIMI EXTRA LAGER.
 
Kundi la Ruau limetwaa ubingwa huo baada ya kupata alama 249 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi.600,000/= na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika julai 20 mwaka huu jijini Mwanza.
 
 Washindi wa pili katika mashindano hayo ni kundi la Abakambamoi ambao wamepata alama 227 na hivyo kujinyakulia fedha taslimu shilingi 500,000/=nafasi ya tatu imechukuliwa na kundi la Rugomoire kwa alama 226 na kuzawadiwa shilingi.400,000/= huku kundi la Aruta wakiondoka na nafasi ya nne na kuzawadiwa shilingi 300,000/= .
 
Jumla ya vikundi 12 vimeshiriki mashindano hayo,ambapo vikundi vingine vilivyo shika nafasi ya 5 mpaka 12 vimeondoka na kifuta jasho cha fedha taslimu sh.150,000/=
 
 Mgeni rasmi katika mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Ziporah Pangani akizungumza na washiriki wa mashindano hayo pamoja na wakazi wa Mkoa wa Kagara waliojitokeza kushuhudia fainali hizo ameipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager kwa kudhamini mashindano mbalimbali na kuvitaka vikundi vilivyo shika nafasi ya kwanza vya Ruau kutoka Karagwe na kundi lililo chukua nafasi ya pili la Abakambamoi kutoka Muleba kwenda kuwakilisha mkoa wa Kagera vema katika mashindano hayo ya Kanda.
 
Ziporah amesema ni aibu kwa mkoa huo kuwa wasindikizaji katika mashindano hayo na kuwataka maafisa utamaduni na viongozi wa vikundi hivyo  kuhakikisha kuwa wanafanya mazoezi kuanzia sasa ili viweze kurejea na nafasi za juu katika  katika mashindano hayo “ nawataka mreje mkiwa nafasi za juu ya kwanza mpaka ya tatu msipo pata nafasi hizo hamto panda meri kurejea kagera”alisema Mkuu wa Wilaya huyo.
 
Naye Meneja masoko  wa Kampuni ya Bia Tanzani  (TBL) Kanda ya Ziwa Andrew Mbwambo amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini  shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa kutumia bidhaa zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea kudhamini shughuli hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao, hasa bia ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa pekee.
 
Aidha Mbwambo amewataka wakazi wa jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi jumamosi hii kushuhudia mashindano hayo ya ngoma za asili na kuwaona wawakilishi wao watakao wawakilisha katika mashindano ya Kanda ambayo yatashirikisha mikoa 6 ya kanda ya ziwa ambapo pia amepongeza mwitikio wa wakazi wa Kagera katika shughuli hiyo.
 
Vikundi vingine ambavyo vimeshiriki katika fainali hizo ni pamoja na Rumanyika kutoka Karagwe, Bikolwengonzi kutoka Bukoba, Tuelimishane kutoka Misenyi, Abasubi kutoka Biharamuro, Jipemoyo Muleba, P. gaigwa, Abaligambo kutoka Bukoba na Obumoi ngonzi .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...