Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 5, 2014

BONDIA IDDI PIALALI AIBEBA KIWANGWA BAGAMOYO KWA KUNYAKUWA UBINGWA WA KANDA YA MASHARIKI
Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Piyalali akiwa na mkanda wa ubingwa wa Kanda ya Mashariki Picha na SUPER D BLOG
Bondia Iddi Pialali

Bondia Iddi Pialali
Bondia Hashimu Zuber kushoto akipambana na Ally Mahiyo wakati wa mpambano wao uliofanyika kiwangwa bagamoyo mkowa wa pwani Zuber alishinda kwa point mpambano huo Picha na SUPER D BLOG
wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia mchezo huo uliopigwa siku ya jumatatu kiwangwa bagamoyo mkoa wa pwani 
Bondia Ally Bugingo kushoto akimtupia konde Twalibu Tuwa wakati wa mpambano wao Bugingo alishinda kwa point
Picha na SUPER D BLOG


Said Yazidu akiongea na mashabiki wakati wa mpambano huo

BAADHI YA WATU AMBAO WALIKOSA KUINGIA UKUMBINI KWA KUTOKUWA NA PESA WAKIPIGA CHAPO KWENYE DIRISHA

Na Mwandishi  Wetu

BONDIA Iddi Pialali mwanzoni mwa wiki hii aliwainuwa mikono juu wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani baada ya kunyakuwa ubingwa wa kanda ya mashariki kwa kumtwanga kwa K,O  ya raundi ya tano bondia Fadhili Mkundi

mpambano huo uliofanyika siku ya jumatatu ulikuwa na shamlashamla nyingi tangia mwanzoni mwa mchezo huo ambapo watu walifulika kuona ndonga zikipigwa Kiwangwa
mpambano huo wa ubingwa ulianza mnamo saa 4 na dakika 20 usiku

uku mashabiki wakimshangilia Pialali kwa furaha mwanzo mwisho raundi ya kwanza ilianza kwa mashambulizi ya kutupiana makonde ya uku na kule ambayo yaliwavutia sana wakazi wa kiwangwa ilipofika raundi ya tatu mashambulizi yakawa kwa upande mmoja ambapo Pialali alibadilisha mchezo kwa kupiga ngumi za tumbo yani juu na chini kufika raundi ya tano Pialali aliongeza mashambulizi hayo kwa kasi na kumfanya refarii wa mpambano huo Pembe Ndava  kumuhesabia mpinzani ambaye alikuwa akivuja damu puani na mdomoni ambapo mpinzani huyo alisalimu amri na Pialali kuibuka kidede kwa kushinda K,O raundi ya tano

kabla ya mpambano huo kulikuwa na mapambano ya utangulizi yaliyowakutanisha mabondia Hashimu Zuber aliyempiga kwa pointi Ally Maiyo na Ally Bugingo alimsambalatisha kwa pointi Twalibu Tuwa


mwisho wa mchezo huo promota wa mpambano huo Bernard Mwakyusa amewahaidi wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo kuwa atapeleka burudani ya masumbwi mara kwa mara kwa kuwa sasa kuna bingwa anayetambulika rasmi katika tasnia ya masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...