Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 24, 2014

LIPUMBA ATAKA PINDA NA WENZAKE WATIMULIWE!


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof.Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu sakata linaloendelea nchini la wizi wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambapo chama hicho kimewata waliohusika kwa namna mbalimbali wajiuzulu au wafukuzwa haraka, akiwataja baadhi alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Warema, Waziri wa Nishati na Madini Pro.Sospeter, Mhongo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, kulia ni Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CUF taifa Yusufu Omari na Naibu Mkurugenzi wa habari na uenezi CUF taifa Abdul Kambaya.
VIONGOZI WA SUDANI KUSINI WAMFUATA KOMREDI KINANA MASASI KUPATANISHWA Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano na baadhi ya viongozi wa makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini ambao wako kwenye mgogoro wa kugombea madaraka kwa takribani mwaka sasa. Kinana amekutana na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara mjini Masasi, Mtwara baada ya kumfuata kutaka ushauri wa upatanishi kutoka kwao Sudani Kuzini. Baada ya ya viongozi hao kupata wasaa wa kusalimia wananchi katika mkutano huo alifanya nao mazungumzo Ikulu Ndogo ya Masasi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG Kinana akiwa katika mkutano wa kuwapatanisha viongozi hao, usiku huu Ikulu Ndogo ya Masasi, Mtwara

Make Money at : http://bit.ly/copy_win
Mbunge wa Kigoma Kusini,mhe david kafulila na jessica kishoa wameremeta mjini uvinza Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014 Mhe David Kafulila akiwa kanisani na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014 Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe Zitto Kabwe na Mhe David Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...