Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 6, 2014

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA


Na Mwandishi Wetu
BONDIA Samsoni Maisha wa kyela amewasili jijini Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa TPBO na Ibrahimu Tamba mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam

mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na

Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...