Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 10, 2014

RAIS WA BUNGE LA SADC NA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MHE. ANNE MAKINDA ASHIRIKI MISA MAALUM YA KUMWOMBEA ALIYEKUWA RAIS WA ZAMBIA MAREHEMU MICHAEL SATA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE LA ZAMBIA MJINI LUSAKA LEO


Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Sata ukiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia leo tayari kwa misa Maalum iliyoandaliwa kabla ya mazishi kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu wa Zambia Mhe. Lupia Banda akimpokea Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda alipowasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda mara baada ya Kuwasili katika Viwanja vya Bunge kushiriki Misa hiyo

3 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...