Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 14, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO KWA WASANII BORA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii ya Mafanikkio katika maisha ya usanii (LIFE TIME ACHIEVEMENT AWARD) Bibi Martina Edward kwa niaba ya Said George Tingatinga kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii bora katika masuala ya kijamii (HUMANITARIAN AWARD) Bw. Patrick Kungalo kwa niaba ya Fr. Canute Mzuanda kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam. Makamu wa Rais alikutana na jopo la waandaaji wa siku ya Msanii, Kampuni ya Haak Neel Production, Baraza la Sanaa la Taifa na Wizara ya Habari, Vijana Michezo na Utamaduni na kutoa zawadi ya fedha shilingi milioni kumi ambazo aliahidi siku kilele cha siku ya Msanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Oktoba 25,2014
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa katika picha ya  pamoja na washindi wa tunzo ya msanii bora na Viongozi wa Wizara ya Habari baada ya kukabidhi tunzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...