Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 14, 2014

JONAS MKUDE ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI SIMBA


Kiungo wa timu ya Simba SC, Jonas Gerald Mkude (katikati) akisani mkataba mpya mbele ya Rais wa Simba , Evans Aveva (kulia), Zachalia Hans Pope (kushoto)
Jonas Gerald Mkude (katikati) akiweka saini ya dole gumba katika mkataba mpya mbele ya Rais wa Simba , Evans Aveva (kulia), Zachalia Hans Pope (kushoto).
KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC na kusema bado nipo sana Msimbazi.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Silver Pippe, Kawe, Dar es Salaam Mkude amesema kwamba amesaini klabu hiyo baada ya kufikia kiwango cha fedha alichotaka.
Mkude mwenyewe hakusema ni kiasi gani amepewa, lakini habari ambazo mtandao huu mezipata zinasema kiungo huyo amepewa Sh. Milioni 60, ingawa mwenyewe alianzia Milioni 80.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...