Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, November 30, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini taarifa ya pamoja ya majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu jijini Nairobi, Kenya jana.
 Baadhi ya washiri wa mkutano huyo kutoka nchini Tanzania......
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...