Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 26, 2012

AZAM YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA AS VITA MABAO 2-1


 Mpira uliopigwa na John Boko ukitinga wavuni na kuandika bao la kwanza.
 Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililofungwa na John Bocco.

TIMU ya Azam Fc, leo imetinga hatua ya Fainali na kumsubiri mshindi kati ya Yanga ya Dar es Salaam ama APR ya Rwanda, baada ya kuichapa AS Vita kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa leo mchana mida ya saa nane katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. 
 
Hadi mapumziko, AS Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Mfongang Alfred, katika dakika ya 34, baada ya kuunasa mpira uliopigwa na Ibrahim Shikanda na kuichambua ngome ya Azam kabla ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Azam, Deo Munishi ‘Dida’.
 
Vita walipata pigo dakika ya 41, baada ya mchezaji wao, Issama Mpeko, kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Azam ilisawazisha bao hilo, kupitia kwa John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 68 aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Kipre Tchetche, kutoka wingi ya kulia.
 
Mrisho Khalfan Ngassa aliyeingia kutokea benchi kipindi cha pili aliifungia Azam bao la ushindi dakika ya 89, akimalizia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Baada ya kufunga bao hilo, Mrisho alikwenda moja kwa moja kwa mashabiki wa Yanga na kushangilia nao, badala ya mashabiki wa Azam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...