Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, July 24, 2012

Matajiri waficha fedha ng'ambo


Utafiti mpya uliofanywa sehemu mbali mbali za dunia, kutaka kujua wapi watu wanaficha fedha zao kukimbia kodi, umegundua kuwa dola kama trilioni 20, zimefichwa nchi za ng'ambo, mbali ya macho ya maafisa wanaotoza kodi.

Ripoti hiyo imeandikwa na shirika la utetezi, Tax Justice Network, ambayo inasema kuwa tofauti baina ya matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivofikiriwa.

Dola trilioni 21 ni sawa na pato la mwaka la Marekani nzima pamoja na Japani.

Tax Justice Network inafikiri fedha zilizofichwa ng'ambo zinaweza kuwa zaidi ya hizo.

Ripoti yao inaonesha jinsi matajiri wakubwa wanavohamisha fedha na kuziweka kwenye nchi zinazoweka siri, kama Uswiswi na Visiwa vya Cayman, kwa kupitia mabenki ya kibinafsi.

Ripoti pia ya inaeleza kuwa nchi zenye utajiri wa mafuta, kama Urusi na Nigeria, ndio hasa kwenye mtindo wa fedha kutoweka na kuvushwa, badala ya kuwekezwa nchini.

Utafiti huo unamaliza kwa kusema wanasiasa sehemu mbalimbali za dunia, wanategemea kuwa fedha hata zikiwa kwa watu wa juu, zitavuja hatimae na kuwafikia maskini - ripoti inasema hayo hayatokei tena.
Chanzo: BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...