Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 30, 2012

WALIMU IRINGA WAKACHA MGOMO, WAIGEUZIA KIBAO CWT, WATAKA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI YA MICHANGO YAO


BAADHI ya walimu wa shule za msingi mjini Iringa wamekigeuzia kibao Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakipinga mgomo wake wa walimu ulioanza nchini kote leo na badala yake wametaka waelezwe kwanza mapato na matumizi ya michango yao ya kila mwezi kwa chama hicho.
“Tunasikia kuna majengo ya walimu yanajengwa nchi nzima, makatibu wa cwt wananuliwa magari, sasa kuna mpango wa kuanzisha benki, lakini hatupewi taarifa ya mapato na matumizi, na hata magari waliyopewa makatibu hayana msaada kwa walimu ambao ndio wenye mali hata kama wakiumwa,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mtwivilla,. Sidified Mapunda.

Alisema mgomo huo unawapa umaarufu viongozi wa chama hicho na hauna maana yoyote kwa walimu wa kawaida kwasababu taratibu za kuongeza mishahara ya walimu hazina tofauti na za watumishi wengine wa umma.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi y a Wilolesi ambayo pia walimu wake wote walisusia mgomo hu, George Kameka alisema kabla ya kumgomea mwajiri wao, wanataka kufahamu tangu kutoka kwa chama chao hicho cha wafanyakazi tangu walimu nchini kote waanze kukatwa asilimia mbili kwa ajili ya kukichangia, mapato na matumizi yake yakoje.

Alisema kuna taarifa zisizo rasmi kwamba CWT iko katika mstari wa mbele kudai maslai ya walimu ili mishahara yao ikipandishwa na wao wapandishe michango yao.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi  ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.

2 comments:

  1. Inaonekana huyo mwalimu anayeuliza asilimia mbili hatimizi wajibu wake hivyo hawezi kudai haki. Yaani sijui anaishi dunia gani. Amuulize mwakilishi wake wa shule mbona kila kitu kiko wazi kuhusu asilimia mbili wanazokatwa

    ReplyDelete
  2. Inaonekana huyo mwalimu anayeuliza asilimia mbili hatimizi wajibu wake hivyo hawezi kudai haki. Yaani sijui anaishi dunia gani. Amuulize mwakilishi wake wa shule mbona kila kitu kiko wazi kuhusu asilimia mbili wanazokatwa

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...