Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 30, 2012

MAMA MWANAMWEMA SHEIN ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE LIMBANI LEO


 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi futari Mzee wa Nyumba ya Wazee Limbani Hamadi Ali, wakati alipofika katika makazi yao kuwatembelea na kutoa  Futari kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati) ni Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawanke na Watoto Bi Zainab Omar. Picha zote na Othman
Maulid,Pemba
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wazee wa Nyumba ya Wazee Limbani Wete Pemba alipofika kuwatembelea na kutoa futari kwa Wazee hao leo.
 Baadhi ya Wazee wanaoishi katika  Nyumba ya Wazee Limbani Wilaya ya Wete Pemba, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipofika kuwatembelea na kutoa futari kwa ajili ya Mwezi  mtukufu wa
Ramadhani leo.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiagana na Viongozi wa Wizara ya Ustawi wa Jamii,  Pemba, baada ya kuwatembelea Wazee wa Limbani Wete na kutoa Futari kwa Wazee hao leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...