Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 28, 2012

SHUHUDIA MATUKIO YANAYOJIRI KWENYE SHINDANO LA EPIQ BONGO STAR SERCH MKOANI TANGA.


Mwana dada Digina Ndetela kutoka Mkoani Dodoma akiwa ametinga tanga kujaribu bahati yake ya kufanya vizuri ili aende Dar es Salaam kushiriki Shindano la Epiq Bongo Star Serch, na hapo akionyesha uwezo wake mbele ya majaji.
Mshiriki huyu anaitwa Mshewa Musa yeye alikosa nafasi Mkoani Arusha na sasa ametinga Mkoani Tanga kujaribu Bahati kwa mara ya Pili.
Washiriki hawa wakiwa kwenye foleni wakisubiri kuingia ndani ya ukumbi kukutana na majaji.
Mshiriki Hidaya Henein akiwa kwenye foleni kusubiri kwenda kuonyesha uwezo wake.

Shindano la Epiq Bongo Star Serch limeingia Mkoani Tanga katika ukumbi wa klabu ya La Casa Chica. Mwamko wa washiriki umekuwa kama ulivyotegemewa ambapo zaidi ya washiriki 300 walikuwa wameisha jisajiri kwanza kwa ajiri ya kufanya usaili siku ya leo. Washiriki wengi walioshindwa kupata nafasi katika mikoa mingine wamejitokeza katika mkoa wa Tanga kitu ambacho kimeongeza ushindani kwa washiriki kutokea eneo hili la Tanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...