Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 25, 2012

NGOZI NA KAZI YANGU VINANIPA DILI...MSANII na mtayarishaji wa filamu za Swahiliwood, Aunty Ezekiel, amesema kuwa matokeo ya kuilinda ngozi yake kwa kutotumia ovyo vipodozi, yamekuwa na faida kubwa kwake.

Anasema kwa umakini huo, ngozi yake ina mwonekano wa kuvutia hivyo kumpa nafasi kubwa ya kupata kazi katika tasnia hiyo.

"Katika maisha yangu, ngozi ina thamani kubwa. Huwa nailinda isidhurike na kemikali, vipodozi vyangu ni vya kawaida kabisa," alisema baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa ZUKU.

"Situmii kemikali kabisa na sina gharama kama wengine, najivunia mwonekano wangu wenye kuvutia pamoja na kuwa na uwezo wa kuigiza, ndiyo maana nawashika wapenzi wa filamu.
"
Msanii huyo pamoja na Jacob Stephen walichaguliwa kuwa mabalozi wa Zuku Swahili Movie inayotarajia kuzinduliwa mwezi ujao.

Kwa ubalozi huo, wanatarajiwa kupata mikataba ya matangazo itakayohusu bidhaa za kampuni hiyo pia kushiriki katika kampeni mbalimbali za filamu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...