Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 26, 2012

Ngoma Africa band kupewa Award ya Kimataifa ! IDA-International Diaspora Award
Habari za uhakika zinaeleza kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" au maarufu kwa jina la "FFU" wazee wa virungu na makombora ya muziki, yenye makao yake nchini Ujerumani,imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza miziki ya Afrika kwa kasi duniani, na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu ya "IDA - International Diaspora Award". Tuzo hiyo inayotolewa na taasisi za kimataifa itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja siku ya Jumapili tarehe 12-8-2012 katika sherehe maalum za Gala Night zitakazohudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mastaa.
Sherehe za kukabidhiwa tuzo hiyo zitafanyika mjini Tubingen, mkoa wa Baden w—Ćrttemberg, kusini mwa Ujerumani.
Taasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanzia mwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya Kiafrika inayolitangaza bara la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu wa kuzipigia kura bendi hizo katika tovuti mbalimbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia ushindi wa mamilioni ya kura, pia imegundulia kuwa bendi hii inakubalika na mamilioni ya mashabiki wa mataifa mbalimbali.
Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni 50 duniani kote, hali hii inatishia mapromota wa muziki wa kimataifa, kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya mashabiki. Katika kambi yao hii www.ngoma-africa.com inakadiliwa kuwa na mamilioni ya wafuasi.
Tunawatakia kila yaliyo mema FFU wetu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...