Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 25, 2012

EXTRA BONGO WAZINDUA ALBAM YA MTENDA AKITENDEWA BARANI ULAYA,SASA IKO SOKONI.BENDI ya Extra Bongo imezindua Albam yao ya Mtenda akitendawa hujihisi kaonewa barani Ulaya katika kipindi hichi ambacho wako safarini Barani Nchini Finland.
Akizungumza kwa njia ya mtandao Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky amesema albam hiyo inajumala ya nyimbo saba ambazo ni Mtenda akitendewa utunzi wake Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chicky,wa pili Falsafa ya Maisha utunzi wake Banza Stone,wa tatu ni Ufisadi wa Mapenzi utunzi wake Robert Hega, wane ni Mashuu utunzi wake Ally Chocky,tano ni Neema utunzi wake Athanas Motanabe,wa sita ni Bakutuka utunzi wake Super Nyamwela na wa saba ni Extra Bongo Shoo.
Albam hiyo kwa sasa iko sokono huko Barani Ulaya na wamefanya hivyo ili kuwaachia  kumbukumbu nzuri wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo Ulaya
Bendi ya Extra Bongo bado inaendelea na maonyesho sehemu mabalimbali wakati huo wakiendelea na tamasha la First Afrika ambalo ndilo mwaliko wao uliowatoa Tanzania.
Bendi ya Extra Bongo iliondoka jijini Dar es Salaam ikiwa na wanamuziki kumi na watano,ambapo Waimbaji watano,upande wa vyombo watano na wacheza shoo watano.
EXTRA BONGO BAND ALBUM
Artists: ALI CHOCKY & EXTRA BONGO BAND
ALBUM: MTENDA AKITENDWA

TRACK LIST:
1. MTENDA - ALI CHOCKY
2. FALSAFA YA MAISHA - BANZA STONE
3. UFISADI WA MAPENZI - ROBERT HEGGA CATERPILLAR
4. MASHUU - ALI CHOCKY
5. NEEMA - ATHANAS
6. BATUKUTA - SUPER NYAMWELA
7. EXTRA BONGO SHOW - BONUS TRACK
Costs: 15€

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...