Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 28, 2012

MKUU WA WILAYA NACHINGWEA AENEZA KAULI MBIUYAKE YA AMANI NA MAENDELEO KWA WANANCHI.


Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Regina Chongo (watatu kulia mrefu) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukutana na makundi ya kijamii likiwemo kundi la kina mama wa wilaya hiyo ikiwa ni kwenye harakati zake za kuhimiza maendeleo Wilayani humo.
Baadhi ya kinamama waliohudhuria mkutano huo wakiongoza na Mee Mashuhuri tangu wakati wa harakati za kudai Uhuru Binti Kanduru (Mwenye Fulana ya Njano) wakifuatilia Mkutano huo Mjini Nachingwea.

OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea imeandaa maombi na kuyapeleka Serikalini kupanga mipango ya Kurudisha usafiri wa Reli ambao ulikuwapo miaka ya nyuma katika wilaya hiyo ili kusaidia Usafirishaji wa Mazao  kama ilivyokuwa awali ambapo tuta la Reli hiyo bado lipo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rigina Chonjo wakati akizungumza na wananchi wa Nachingwea ikiwa ni sehemu ya harakati zake za kuhimiza maendeleo.
Kupitia kauli mbiu yake ya Amani na Maendeleo amewahimiza wakazi wa Wilaya hiyo kufanya kazi  kwa juhudi ili kujiongezea kipato. Pamoja na kuwahimiza wawekezaji kujitokeza kuwekeza kwenye Wilaya hiyo kuna fursa nyingi ikiwemo madini ya aina mbalimbali.
Alihimiza kila kijana mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kazi asikae bila ya kazi hasa ukizingatia shughuli kuu za kiuchumi wilayani humo ni kilimo, Kwa upande wa wazazi wao wamehimizwa kufuatilia na kusimamia elimu ya watoto wao

1 comment:

  1. Lakin wilaya yetu ya Nachingwea miundombinu yake hata suala la elimu kwa mazungumzo alisaidii,jambo la msingi ni vitendo,ukiangalia wilaya ya Nachingwea hakuna hata shule 1 ya form 5-6,na hakuna hata elimu kwa wananch,je tutafika?

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...