Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 28, 2012

TCRA YATOA UFAFANUZI WA SATELITE
MWINGILIANO wa masafa ya televisheni uliotokea hivi karibuni katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Mbeya umeelezwa kusababishwa na masafa yaliyokuwa yakitumika kuchukuliwa na wamiliki wake halali walioyanunua.

Hayo yamebainishwa leo na Meneja wa mamlaka ya mawazsiliano nchini(TCRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Deogratius Moyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Moyo amesema kuwa masafa hayo  hivi sasa yanatumika kutolea huduma za Interneti kwa makampuni yanayotoa huduma hiyo nchini.

Amesema kwa watumiaji  wa dishi ya Setilaiti wanatakiwa kufanya marekebisho ya madishi yao ili waweze kupata masafa sahihi yanayorusha matangazo kwenye masafa yaliyotengwa kwa ajili ya matangazo
 ya Televisheni.

Akifafanua zaidi, Meneja huyo amesema masafa ya sataelaiti katika C-Band huanzia 3.7GHZ hadi 4.2GHZ yametengwa kwa ajili ya intaneti barani Afrika huku masafa hayo katika C- Band huanzia 3.4GHZ hadi 3.6GHZ ni kwa ajili ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumzia tatizo la masafa katika jiji la Mbeya, Moyo amesema kuwa kwa kuwa wananchi wengi walifunga kifaa cha kunasa mawimbi (NLB) kwenye uelekeo wa masafa ya intaneti ambayo wamiliki wake walikuwa hawajaanza kuyatumia, na kuwa baada ya wamiliki halali kuyachukua imesabaisha baadhi ya watu kukosa matangazo ya televisheni.

Meneja huyo amesema masafa hayo kwa hivi sasa yanatumiwa na kampuni ya simu ya Vodacom, hivyo watumiaji wengine hawana budi kuhama na kubadilisha kifaa cha kunasa matangazo kwa njia ya sataelaiti (LNB).

Amesisitiza wananchi kujiunga na mfumo wa digitali kwa kuwa ifikapo Desemba 31, mwaka huu mitambo ya kurushia matangazo kwa njia ya analojia itazimwa nchini huku akiusifia mfumo mpaya akisema ni salama, hauna madhara wala  gharama kubwa kwa mtumiaji.

Kwa hisani ya Joachim Nyambo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...