Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 30, 2014

THOMAS MASHALI AJIUNGA RASMI NA TASWA FC SASA KUANZA KUWAPA MAUJUZI YA NDONGA WANATASWA


 Mwenyekiti wa Taswa Fc, Majuto Omary, akimtambulisha Rasmi, Bondia Thomas Mashali, aliyejiunga na timu hiyo siku ya jumamosi katika mazoezi yanayofanyika kila jumamosi kwenye uwanja wa Chuo cha Ustawi, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. 

Katika kujitambulisha Bondia huyo pia ameweka mikakati ya kuanzisha timu ya ngumi katika kikosi hicho cha Taswa, ambapo tayari baadhi ya wachezaji wameonyesha kuvutiwa na mpango huo na kuonyesha nia ya kushiriki kikamilifu mazoezi hayo ya ngumi yatakayokuwa yakianza mapema siku ya jumamosi kabla ya kuanza mazoezi ya soka.

Miongoni mwa wachezaji wa Taswa waliothibitisha kuanza mazoezi ya ngumi na kushiriki katika baadhi ya mapambano ya ngumi yatakayokuwa yakiandaliwa na mapromota au Taswa wenyewe, ni pamoja na Hussein, Lukonge, Mkongwe, Niku, Jimmy, Deusi na Super D
Majuto Omary, akiendelea kumtambulisha Mashali....

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...