Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 19, 2014

WASHINDI WA CHEMSHA BONGO YA BRAZIL WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatano, Phillip Nkini (kulia) akimkabidhi Said Muhammed Muba zawadi yake ya dekoda na dishi.
Ofisa Mauzo wa Azam TV, Shah Seffu Mrisho (kulia)  akimkabidhi Allen John Muhuma zawadi ya TV na dekoda.
Ofisa Usambazaji wa Global, Benjamin Mwanambuu (kushoto) akiwa katika pozi na washindi Allen na Said pamoja na Nkini na Shah.
Washindi wa Chemsha Bongo ya Brazil, Said Muhammed Muba (kushoto) na Allen John Muhuma wakiwapozi na zawadi zao.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Innocent Mafuru (kulia) akipozi na washindi wa Chemsha Bongo ya Brazil. Kushoto ni Benjamin Mwanambuu na Ofisa Matukio na Mitandao ya Kijamii wa Azam TV, Irada Mtonga (katikati).
Allen John Muhuma akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani).
Ofisa Usambazaji wa Global, Benjamin Mwanambuu akielezea jinsi ya kushiriki Chemsha Bongo ya Brazil inayoendeshwa na magazeti ya Championi kwa udhamini wa Azam TV.
Said Mohammed Muba akipozi na dekoda yake.
Washindi hao baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

WASHINDI wa Chemsha Bongo ya Brazil ambayo inadhaminiwa na Azam TV, Allen John Muhuma na Said Mohammed Muba, wamekabidhiwa zawadi zao leo kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar.

Washindi hao ambao walifanikiwa kujibu ipasavyo maswali kwenye swali la Chemsha Bongo lililokuwa kwenye magazeti ya Championi ya wiki iliyopita, wamejishidia TV, dekoda ya Azam na dishi.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao walisema kuwa hii ni faraja kubwa sana kwao kwa kuwa wameweza kuboreshewa maisha yao na Championi. “Ukweli hii ni faraja kubwa sana kwangu na familia yangu, nimejisikia vizuri sana na kamwe sitaacha kushiriki kwenye kila toleo,” alisema Muba. Kwa upande wake Muhuma, alisema awali aliamini kuwa kuna watu huwa wanaandaliwa kwa ajili ya kushinda zawadi hizi.

“Hili limenifanya niamini kuwa Chemsha Bongo hizi ni za kweli, nimefarijika sana na niahidi kuwa nitashiriki kila siku na naamini nitashinda tena.” Ukitaka kushiriki Chemsha Bongo hii jibu swali ambalo lipo kwenye gazeti la Championi kisha tuma jibu lako kwenda namba 15564, hapo utakuwa umeingia moja kwa moja kama mshindani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...