Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 19, 2014

WORLD CUP 2014: GHANA 1 v UNITED STATE 2, CLINT DEMPSEY AWEKA HISTORIA...AFUNGA BAO LA MAPEMA..SEKUNDE 29! JOHN BROOKS AKIWAFUNGIA U.S BAO LA USHINDI!!


John Brooks alifunga Bao la Kichwa Dakika 4 kabla Mpira kumalizika na kuipa USA ushindi wa Bao 2-1 kwenye Mechi ya Kundi G iliyochezwa huko Estadio das Dunas Jijini Natal Nchini Brazil. 
USA walitangulia kupata Bao Sekunde ya 29 tu, hili likiwa ni Goli la 5 la mapema kwenye Historia ya Kombe la Dunia, alilofunga Clint Demsey, Mchezaji wa zamani wa Fulham. 
Andre Ayew aliisawazishia Ghana Dakika ya 82 baada kupokea Pasi ya Kisigino ya Asamoah Gyan.
Biashara mapema: Clint Dempsey akishangilia vikali baada ya kuifunga Ghana bao la baridi...mapeeema!!
Dempsey akiruka juu baada ya kuziona nyavu za Ghana hapa Natal
 Dempsey akipongezwa na wenzake kwenye kona ya uwanja..
Mashabiki wa USA wakishangilia kwa aina yao...Scarf juu
Dempsey ilikuwa kama sekunde 29 mpaka 31 kitu 1-0
Dada akishindwa kujizuia...yeye na USA damu damu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...