Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 4, 2014

POLISI FEKI WAKAMATWA MKOANI IRINGA




Kamanda wa  polisi mkoa wa Iringa,Ramadhan Mungi akiwaonyesha maaskari  feki ambao  walikuwa wakifanya utapeli katika mikoa ya Iringa na Morogoro ,kulia ni Bazil Nyakunga ambae ni mwalimu akiwa na sare za polisi na katikati ni bossi wake Godlack Mbehale.
Askari polisi Mkoani Iringa (kushoto) akiwa na maaskari  feki katika ofisi ya kamanda wa polisi  leo 


Na Francis Godwin,Iringa

MATAPELI washindwa  kubaki njia  kuu sasa waanza  michepuko  mipya ni baada ya jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa kumkamata  mwalimu aliyejifanya askari akiwa na fullu kombati za jeshi la polisi na  bossi wake aliyevalia kiraia ambae pia ni  feki  na ni  mmiliki wa studio eneo la Kihesa mjini hapa.

Upo usemi  usemao  kuwa usiombe  likukute usilo litegemea kukukuta katika maisha yako na ukipenda kudanganya uwe tayari kudanganywa  ,hakuna asiyepata  kusikia ama kusoma habari kuhusu utapeli  unaoendelea hapa nchini kwa  watu wa kada mbali mbali na mazingira  yanaonyesha matapeli hawa  siku  zote ni watu  wanaopenda wengine yawakute na sio  wao na hata kupenda kudanganya na sio kudanganywa kama ambavyo mwalimu huyo Bazil Nyakunga (20) ambae anatuhumiwa  kutapeli  wazazi wengi Iringa na Morogoro ambao  wanataka  watoto wao kwenda kusomea uaskari .

Mwalimu Nyakunga  akiwa na bossi  wake  feki Godlack Mbehale (21) walijikuta matatani kwa  kukutwa na wasilotegemea  kulipata  baada ya  jeshi la  polisi kuweka mtego kufuatia wananchi wengi kufika  polisi  kulalamikia utapeli huo wa  ajira  kwa vijana  wao katika  jeshi la  polisi.

Ramadhan Mungi ni kamanda  wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa alilitonya gazeti  hili kuwa jeshi  lake  lilipopata stori   hiyo ya utapeli  waliweka mtego eneo la Ipogolo ambapo askari huyo feki alikuwa amepiga kambi la kitapeli kwa  kuwasanua mavumba wazazi wenye uchu wa  watoto  wao kuwa mageda (ma Askari).

Alisema  kuwa  vijana  hao ambao  mmoja  Nyakunga ambae ni mkazi wa Ilula Mtua katika  wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ni kijana  aliyepata  kusoma kozi ya ualimu mkoani Shinyanga  na kuwa ndie  alikuwa akijifanya na askari  polisi na muda  wote  alikuwa akivaa sare za jeshi  hilo.

Mungi  alisema  kuwa  kijana  huyo na mwenzake  wamepata  kuwaliza  watu wengi  sana Iringa na Morogoro na  kuwa mtu wa mwisho  wamemliza kiasi cha Tsh 900,000 na kuwa njia  wanayotumia ni Nyakunga kama askari  baada ya  kumpata  mazazi na mtu mwinye uhitaji na ajira ya  polisi amekuwa akipiga simu kwa boss  wake Bw Mbehale na kuiweka simu hiyo katika mfumo wa Laudi spika ili mtu anayetapeliwa  kupata  kusikiliza vema mazungumzo hayo.

“ Nyakunga kama askari  feki  baada ya  kumpata mteja  wa kumtapeli amekuwa akiweka simu yake katika  sauti  kubwa na huyo boss  wake amekuwa akisikika akipanga gharama za mtapeliwa  kulipia na baada ya  kutoa  pesa  wamekuwa  wakiingia mitini kwa kumta ahadi feki….mfano anapopiga simu anajifanya samahani boss naomba maelekezo ya mwisho huyu mzazi /kijana anataka kazi anapaswa kutimiza nini kwa  sasa kabla ya kuitwa katika usaili ”.

Hata  hivyo kamanda Mungi alisema  kuwa ni  vema  wananchi kuchukua  tahadhari juu ya utapeli huo na kuwa kazi za polisi kwa  sasa haziingizwi kwa mtindo huo na kuwa jeshi  hilo lina utaratibu wake wa kuingiza  vijana ikiwa ni pamoja na kuwachucha toka  sekondari  kwa kujaza fomo huku wale  wa elimu ya  juu  upo utaratibu na  wale  wanaochukuliwa kwa utaalam  wao pia  wanautaratibu wao  na si vinginevyo.

Alisema  kuwa  hakuna  usaili  wa askari  unaofanywa  mitaani ama  wilayani  hivyo vijana  hao  walikuwa  wakifanya utapeli  na ni vema  wananchi  kuchukua tahadhari  kubwa .

Pia  alisema jeshi lake  linafanya uchunguzi  ili  kubaini eneo  ambalo matapeli hao  walipata  sare  hizo za  jeshi la  polisi na mbinu  waliyotumia  kuzipata sare  hizo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha  mahakamani.

Hata  hivyo kwa  upande wao matapeli  hao  walidai kuwa   ni kweli  wanafanya kazi na ualimu na mmoja na mmiliki wa  studio eneo la Kihesa mjini  Iringa na  kuwa sare  hizo  walizipata kutoka kwa rafiki yao ambae ni askari polisi aliyewatuma kuzifikisha kwa ndugu yao askari .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...