Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 12, 2014

SOMA TAARIFA MAALUM KWA UMMA KUTOKA KAMPENI YA RELI TANZANIA- TRL KUHUSU KUSITISHWA KWA MUDA HUDUMA YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kutetereka kwa  daraja la reli kati ya stesheni ya Ruvu na mchepuko wa reli ya Ruvu kwenda Mruazi usiku wa kuamkia leo, umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa  daraja utakapokamilika.
Tokea asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini kuwa linahitaji kuimarishwa  ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.

Kwa taarifa hii  wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla  ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya leo  Juni 10, 2014 wanatakiwa kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili watafute usafiri mbadala.

 Aidha Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na
Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL 
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam
Juni 10, 2014

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...