Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 8, 2014

TIMU YA MBEYA CITY FC YAPATA MDHAMINI RASMI AMBAO NI BINSLUM TYRE COMPANY LIMITED.


 kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel na mkurugenzi wa kampuni ya Binslum Tyre wakionesha flana zenye nembo ya kampuni ya Binslum Tyre kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro,alisema Halmashauri imepata faraja kubwa kupata mdhamini kutokana na Halmashauri kutokuwa na fedha za kutosha kuweza kuendesha timu.

Mkurugenzi wa kampuni ya Binslum Tyre , Mohamed Binslum akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Mbeya

Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya

Wakuu wa Idara


 Katibu wa Timu ya Mbeya city, Emmanuel Kimbe, akiishukuru kampuni hiyo kwa udhamini wa timu yao ya Mbeya city


Add captionTIMU ya Mpira wa miguu ya Mbeya City Fc inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeanza kujihakikishia kufanya vizuri zaidi kwa msimu ujao baada ya kupata rasmi mdhamini.
Kampuni ya Bin Slum Company Limited yenye makao makuu jijini Dar Es Salaam ndiye kampuni ya kwanza kukubali kuwa mdhamini wa timu hiyo kwa miaka miwili kwa kitita cha shilingi Milioni 360.
Utilianaji sahihi wa  mkataba umefanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mbeya baina ya Uongozi wa Kampuni hiyo na Halmashauri ya Jiji la Mbeya mbele ya vyombo mbali mbali vya habari.
Akizungumza na vyombo vya habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohamed Binslum, alisema kampuni yake imefikia makubaliano hayobaada ya kuridhika na uongozi wa Mbeya city namna ulivyojipanga katika kuendesha timu.
Binslum alisema pia kampuni yake imeridhika namna timu hiyo ilivyopata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Jiji la Mbeya pamoja na mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Aliongeza kuwa katika mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 360  kampuni hiyo itakuwa ikitangaza bidhaa zake ambazo ni RB Battery katika Jezi za Timu ya Mbeya city na nyuma ya jezi chini ya namba itaandikwa jina la kampuni la Binslum Tyre Company.
Mkurugenzi huyo alisema kuingia Mkataba na Mbeya city ni fursa pekee ya Kampuni kutangaza bidhaa zake za Betri aina ya RB ambazo zina soko kubwa Mkoani Mbeya pamoja na bidhaa zingine ambazo ni matairi aina ya Double star na vee rubber.
Kwa upande wake Katibu wa Timu ya Mbeya city, Emmanuel Kimbe, mbali na kuishukuru kampuni hiyo kwa kukubali kuwa mdhamini wa Mbeya city pia alimuahidi kutekeleza kile mdhamini anachotarajiwa kukipata kwenye timu hiyo.
Alisema Mbeya city inadhumuni la kutangaza bidhaa za Bin Slum kupitia jezi za mechi za  ndani, Nje na mazeozi ikiwa ni pamoja na timu kuendelea kufanya vizuri.
Aliongeza kuwa mbali na kupata mdhamini lakini wamiliki wa timu pia wataendelea kufanya majukumu yao kwa ajili ya timu kama kawaida na kuongeza kuwa mkataba huo unaanza Juni Mosi Mwaka huu hadi Mei 31, 2016.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro,alisema Halmashauri imepata faraja kubwa kupata mdhamini kutokana na Halmashauri kutokuwa na fedha za kutosha kuweza kuendesha timu.
Alisema kuendesha timu kunahitaji kuwa na uchumi mkubwa ambao Halmashauri haina hivyo kupitia mdhamini huyo timu ya Mbeya city itafanya vizuri zaidi katika msimu ujao.
Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...