Katibu mkuu wa Tanzania Professional Boxing Organisation (TPBO)
Ibrahim Kamwe ambaye anajulikana kwa jina la bigright amejitoa katika uongozi wa chama cha ngumi kama
kiongozi.
Bigright ambae ukiondoa mambo ya kichama mara nyingi amekuwa
akiwaongoza maofisa wa chama hicho katika shughuli mbalimbali na mapambano
mengi kama jaji mkuu ,muhifadhi rekodi za mabondia na mshauri katika shughuli
za kiufundi.
Akizungumza na vyanzo vya habari amesema ameamua kupumzika
shughuli za TPBO na kurudi kwenye ufundishaji wa vijana na kuendelea na kampuni
yake ndogo ya bigright promotion ambayo inajihusisha na utayarishaji wa
matamasha na uandaaji wa mapambano ya ngumi. ‘ kwa kuwa naupenda mchezo wa
ngumi nimefanya shughuli hii kwa muda
mrefu kukiwa na utatautata wa hapa na pale na yote hii kwa ajili ya kuuendeleza mchezo
wa ngumi nchini lakini imekuwa ni ngumu kwangu kuendelea na wadhifa huo ,
nawashukuru maofisa wenzangu wamekuwa wakinipa ushirikiano wa karibu. Ila kwa
sasa najitoa katika uongozi na nitajihusisha na ngumi kivingine ikiwemo
kuwaendeleza vijana na kuandaa mapambano madogomadogo ya kukuza vipaji
No comments:
Post a Comment