Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 12, 2013

SUNDERLAND YA UINGEREZA YAPANIA KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA NCHINI KWAO


 Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson(kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam  juu ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo (kushoto).
Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) akimkabidhi jezi ya timu yake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo (kushoto) leo jijini Dar es salaam mara baada ya mazungumzo ya awali ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...