Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 12, 2013

Walimu wajiandaa kugoma tena, kisa deni lao la Sh Bil 33


http://4.bp.blogspot.com/-mPShZB4Y4hw/UCTkxuUbr2I/AAAAAAABaRs/AB1UTstJ4qk/s640/1.jpg
WALIMU nchini wameipa serikali muda wa mwezi  mmoja kabla ya kuingia tena kwenye mgomo kwa ajili ya kushinikiza walipwe malimbikizo ya madeni yao yanayofikia Sh. Bilioni 33.
Tishio hilo limetolewa na uongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambapo kimesema kinatoa muda wa mwezi mmoja tu kwa serikali kuweza kulipa fedha hizo la sivyo wataingia kwenye mgomo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa chama hicho, 
Gratian Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.

‘Tumetoa mwezi huu wa tisa uwe wa mwisho kuililia serikali, baada ya hapo tutaamua hatua gani tufanye, maana tumekutana na makatibu wakuu wa wizara zinazowahudumia walimu lakini bado tunaishia kupewa ahadi hewa,” alisema Mukoba.

Mukoba aliongeza kuwa Agosti 14, mwaka huu, walikutana na makatibu wakuu wanaowahudumia walimu pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma, wakatakiwa kuwasilisha madai yao yote.

“Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho, tuliwafahamisha kuwa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 33 na mwisho wa kikao hicho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili,” aliongeza Mukoba.

Mukoba alisema wiki mbili zilipofika, walienda kuonana tena na Katibu Mkuu, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuwasilisha vitabu vyenye madai mbalimbali ya walimu.

“Madai hayo tuliyaambatanisha kwenye barua Na CWT/004/UTMS/VOL.11/94 na madai hayo sasa yamefikia sh bilioni sita,” alisema Mukoba.

Mukoba aliishangaa serikali kuanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now”, huko walimu ambao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo, wana maisha magumu kutokana na mishahara kuwa midogo na kuzidi kwa malikimbizo ya madeni yao.

“Walimu ambao ndiyo watelekezaji wakuu wa mpango huu japo hawaelewi au hawajapewa semina elekezi, lakini ndio watekelezaji wakubwa.

Naishangaa serikali kuwadharau walimu na nakuhakikishia mpango huo hautafanikiwa kama walimu hawapati haki zao,” alisema Mukoba.

Mukoba aliionya serikali ikamilishe madai ya walimu ili wafanye kazi kwa moyo tofauti na sasa ambapo wengi wamekata tamaa.

‘‘Walimu wa nchi hii wamekata tamaa. Mioyo yao imekufa ganzi kwa sababu serikali imekataa kuwalipa malimbizo yao.

Kwa nini serikali imeamua kuwatendea jeuri walimu kiasi hiki?” alihoji Mukoba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...