Madawati zaidi ya 1000 yaliyotengenezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Butuguri iliyopo katika Halmshauri ya Musoma mkoani Mara yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi shuleni hapo.
Akiongea na waandishi wa habari Mbunge wa jimbo la
Musoma Vijijini Nimrod Mkono alisema kuwa kumekuwepo na wizi mkubwa katika
miradi mbalimbali ya TASAF hivyo hayuko tayari kuona wizi huo unaendelea katika
jimbo hilo
Alisema
miradi iliyotengenezwa na Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii haifai
ikilinganishwa na shule hiyo ya Butuguri aliyoijenga kwa fedha zake,huku wezi
wa fedha za mfuko huo wakiendelea kulindwa
Mh Mkono amesema kuwa kumekuwepo na desturi ya
kumkamata mwizi wa kuku na kumua lakini watu wanaoiba na kutumia fedha za Umma
vibaya wakiachwa bila kukamatwa.
Mbunge huyo akionyesha kukasirika kutokana na
ubadhilifu huo wa fedha za Madawati hayo alisema atabeba madawati hayo na
kuyarudisha katika halmashauri hiyo na yeye kuleta madawati mengine kwa
matumizi shuleni hapo
Aidha madiwani kutoka Halmashauri hiyo Luti Mayamba
na Thomas Nyasiro waliokuwa wameambatana na Mbunge huyo wamesema vitendo hivyo
si vya kiungwana kwani inaonyesha dhahiri viongozi wanavyotumia madaraka yao
vibaya na kuahidi kufika suala hilo katika baraza la madiwani ili hatua stahiki
zichukuliwe.
Madawati hayo zaidi ya 1000 yaliyotengenzwa na MfuKo
wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa zaidi ya shilingi milioni 50 chini ya aliyekuwa
mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Dr Karnai Kunei yameharibika
muda mfupi mara
baada ya kuanza kutumika.
No comments:
Post a Comment