Mshambuliaji
wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Dany Mrwanda (kulia)
akichuana kuwania mpira na Nahodha wa URA ya Uganda, wakati wa mchezo wa
timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo timu ya
Simba imefungwa mabao 2-0 na kutoa picha iliyo sawa na watani wao wa
jadi Yanga, ambao nao pia katika mchezo wao wa jana walichapwa mabao 2-0
na Atletico na kuwaacha mashabiki wa timu hizi mbili wakibaki na
maswali mengi yasiyo na majibu.
Mchezaji
wa timu ya URA ya Uganda, Derrick Walulya (kushoto) aliyetemwa na Klabu
ya Simba msimu ujao akimhadaa mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu,
wakati wa mchezo wa kuwania kombe la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho
la Vyama vya michezo Afrika Mashariki CECAFA.
Mchezaji mpya wa Simba, akiwatoka mabeki wa URA wakati wa mchezo huo leo jioni. Picha na MdauT
No comments:
Post a Comment