Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 20, 2013

KASEBA,ALIBABA KUPIMA UZITO FRIENDS CORNER HOTEL KESHO



Mabondia jafet kaseba wa jijini Dar es salaam na Alibaba Ramadhan wa arusha wanategemea kupima afya na uzito kesho jumamosi ya tarehe 21 decemba 2013 saa nne asubuhi katika ukumbi wa friends corner hotel ambapo ndipo hapohapo pambano lao litafanyikia siku inayofuata ya jumapili tarehe 22/12/2013 kuanzia saa kumi jioni

Pambano hilo liloandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya  BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya karage suba na bondia mkali anaechipukia kwa nguvu  Fadhili awadh[tiger]  katika uzito wa wealter[66kgs] pambano la raundi kumi, nao wanategemea kupima hiyo kesho

kizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa  mabondia wanaotegemea kupima ni mbaruk heri mabae  atapima kwa ajili ya kuzipiga na lusekelo daudi ,Issa omar nampepeche na Hassan kiwale’moro best’, Zumba kukwe na Jacob maganga, Adam Yahaya na Harman shekivuli, jocky hamis na mbena rajab, Ernest Bujiku na Shah kasim, shaban bodykitongoji na mwinyi mzengela, shaban manjoly na  kasim chuma.

Nae Mtanzania aishie Canada kareem kutch  atapima na  Tata boy kwa ajili ya pambano la kimataifa la mchezo wa kickboxing la raund tano, Mabondia wote wameshawasili Dar es salaam, wakati Alibaba Ramadhan wa Arusha na Jacob maganga wa Tanga wamefikia katika hotel ya valley view wakati kareem kutch yupo Durban hotel kariakoo wapo vema na wenye furaha kwa mapambano yao

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...