Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 17, 2013

KONGAMANO LA VIONGOZI WANAWAKE AFRIKA KUFANYA BONANZA KESHO UWANJA WA TAIFA




Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Amosi Makala (kushoto) akipongezwa na mmiliki wa Taasisi ya Right to Play, Dr. Dennis Bright (kulia) baada yakufungua kongamano la wanawake wa Afrika viongozi wa michezo linalofanyika nchini



Nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake, ‘Twiga stars’, Sophia Mwasikili akiwatambulisha wachezaji wenzake (hawapo kwenye picha) kwenye kongamano la wanawake wa Afrika viongozi wa michezo

Mmiliki wa Anita Foundation, Dr. Anita White akizungumza kwenye kongamano la wanawake wa Afrika viongozi wa michezo lililofanyika nchini. Waliokaa wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Amosi Makala kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Ole Gabriel na mmiliki wa Taasisi ya Right to Play, Dr. Dennis Bright na mwisho ni Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo

WASHIRIKI wa kongamano la wanawake viongozi wa Afrika linalofanyika nchini leo watafanya bonanza la michezo yote katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza na Habari Leo, Kaimu Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambaye ndiye mwandaaji wa kongamano hilo  Juliana Yasoda alisema kuwa watafanya bonanza hilo ambalo litajumuisha michezo yote katika Uwanja wa Taifa kuanzia saa 3:00 asubuhi.
“Kesho (leo) tutafanya bonanza ambalo litahusisha michezo yote kwani hapa kuna viongozi na wanamichezo wa michezo yote na baadae timu za Taifa ya Twiga na ile U-20 watacheza mchezo wa kirafiki”, alisema Juliana.
Michezo ambayo itachezwa ni soka, riadha, kikapu, mikono, wavu, magongo, kurusha tufe na kisahani pamoja na kuvuta kamba.
Pia alisema kongamano hilo limesaidia kutoa mwanga na dira kwenye michezo miongoni mwa washiriki kutokana na kila mmoja kuelezea uzoefu wake katika michezo ukilinganisha na sera za nchi anayotoka.
Awali juzi wakati akifungua kongamano hilo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makala aliwataka washiriki hao kupigania michezo katika nchi wanazotoka  kwani wanawake ni chachu ya mafanikio kwenye michezo mbalimbali hasa wakipewa elimu ya maendeleo ya michezo.
Kongamano hilo lilikuwa la siku mbili na lilishirikisha viongozi wanawake toka nchi za Msumbiji, Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda, Zambia na  Ghana  pamoja na wageni wengine toka Finland na Marekani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...