Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 20, 2013

OKWI ALIVYOPOKELEWA KIFALME NA MASHABIKI WA YANGA HADI MAZOEZINI KUJIANDAA NA MCHEZO WA KESHO DHIDI YA SIMBA Mchezaji wa Kimataifa Emmanuel Okwi (kulia) akijumuika na wachezaji wenzake wa Yanga katika mazoezi yao yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kijitonyama leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa 'Nani Mtani Jembe' dhidi yao na Simba unaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Okwi amewasili jana jioni na kupokelewa kifalme na mashabiki wa Yanga hadi Klabuni mitaa ya Jangwani na kutambulishwa kwa mashabiki na kisha leo kujumuika na wenzake katika mazoezi ya pamoja.
 Emmanuel Okwi (katikati) akiwa na wachezaji wenzake katika mazoezi ya pamoja kwenye Uwanja wa Kijitonyama, leo asubuhi.
 Mazoezi yakiendelea.
 Wachezaji wakipata maji baada ya mazoezi...
 Okwi akizungumza jambo na kocha mkuu wa Yanga Brants.
 Sehemu tu ya mashabiki wa soka waliofurika kwenye uwanja wa Kijitonyama kumshuhudia Okwi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...