Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 12, 2014

CCM YAMTEUA GODFREY WILLIAM MGIMWA KUPEPERUSHA BENDERA YAKE KATIKA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA


Kamati Kuu ya CCM, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Godfrey William Mgimwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.

   Akizungumza na waandfishi wa habari leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katribu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Kamati Kuu ya CCM  imemridhia Godfrey kupeperusha bendera ya CCM baada ya kukidhi vigezo licha ya kuongoza katika kura za maoni jimboni humo.

   Godfrey ni Mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga na pia Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa ambaye ameliacha wazi jimbo hilo baada  kufariki dunia Januari 1, 2014.    Pichani, Nape akimtambulisha Godfrey kwa waandishi wa habari, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Imetayarishwa na theNkoromo Blog  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...