Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, February 15, 2014

MPANGO WA KUBORESHA TAIFA STARS WAIVA, ILA KIM HATAUSIKA



Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamali Malinzi, (katikati) akiongea na wandishi wa habari kuhusu Mpango Maalum wa Kuboresha timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ katika Ofisi za Shirikisho hilo zilizopo katikati ya jiji. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na kulia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZDF), Ravia Idarous.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza mikakati ya kuiwezesha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kufuzu kwa Fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani baada ya kupanga timu hiyo kuweka kambi nchini Uholanzi.

Kambi hiyo maalumu kwa timu hiyo itasaidia kujiandaa na hatua ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco na kushirikisha jumla ya mataifa 16 yatakayofuzu.


Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema endapo Stars itafanikiwa kupita katika hatua ya awali ya mchujo ikiwa itapangwa kwenye hatua hiyo, wamepanga kuweka kambi nchini Uholanzi ili kujiandaa na hatua ya pili ya makundi.

Malinzi alisema wameamua kufanya hivyo ili kurudia historia ya mwaka 1979 ya Stars kufuzu kwa mara ya mwisho michuano ya AFCON, iliyofanyika nchini Nigeria, kwani Stars iliweka kambi Uholanzi kufanikiwa kufuzu kwa fainali hizo.

“Tumepokea barua ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) inayotueleza kuwa mechi zetu za mchujo zitaanza kati ya mwezi Mei hadi Agosti kutokana na kiwango chetu kuwa chini ya nchi 21 bora za bara hili, hivyo muda si mrefu tunafikiria kurekebisha benchi lote la ufundi kwa pamoja na kuanza mikakati ya timu hiyo.

“Huenda timu yetu ikaanzia hatua ya mchujo kama CAF walivyotuandikia, ikifanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi ttumepanga kuweka kambi nje ya nchi katika nchi ya Uholanzi, na huko timu itapata mafunzo ya kisasa ili kufanya vizuri kwenye hatua ya makundi,” alisema Malinzi.

Pia alisema wameshazungumza na Balozi wa Uholanzi hapa nchini kwa ajili ya mipango yao hiyo, pia wamewataarifu wadhamini wakuu wa Stars, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Kilimanjaro Premier Lager ili kuandaa bajeti ya ziara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...