Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 27, 2014

NMB YASOGEZA HUDUMA KARIBU ZAIDI NA WAKAZI WA BARABARA YA MANDELA



Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Bw. Meck Sadick akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mandela Road .Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam ,Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni  Mkuu  wa kitengo cha Huduma kwa wateja wakubwa  NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.

NMB yazindua tawi jipya barabara ya Mandela mkoani Dar es Salaam.Hili ni tawi la ishirini  na tatu kufunguliwa katika mkoa wa Dar es Salaaam, na hii inafanya NMB kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania, ikiwa na matawi zaidi ya 150 yaliyosambaa nchi nzima.


Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay akimwelezea  Mheshimiwa Mmkuu wa mkoa wa Dar es salaam (kwanza kushoto ,Bw. Meck Sadick huduma mbali mbali zitolewazo na tawi jipya la NMB mandela Road


Tawi hili la NMB Mandela Road, linatoa huduma mbali mbali za kibenki ikiwemo akaunti za akiba, mikopo , huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipia kwa niaba  ya serikali na taasisi mbalimbali. Tawi hili litakua wazi kila  Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili  na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi - 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Bw.Meck Sadick (kwanza Kushoto akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana ,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.


Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya. Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. 



Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw. Meck Sadick (pili kulia kwenye viti) akiwa kwenye picha ya Pamoja na maafisa wa NMB tawi la Mandela Road.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...