Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 10, 2014

MTEMVU AZUNGUMZA NA HALMASHAURI KUU YA CCM KATA YA BUZA KUHUSU UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM NA UTATUZI KERO ZA WANANCHI


 Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam,  Abbas Mtemvu  akiwasili katika ukumbi wa Mihogoni, Kata ya Yombo Buza, katika jimbo hilo, kwa ajili ya kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Buza kwa ajili ya kujadiliana nao hali ya utekelezaji wa ilani ya CCM na kero zinazowakabili wananchi katika jimbo hilo,leo.
 Wajumbe wakiwa wamesimama baada wa Mtemvu kuingia ukumbini
 Watendaji katika Idara mbalimbali katika Kata hiyo wakiwa wamesimama kumlaki Mtemvu
 Katibu wa CCM, Kata ya Buza Shabani Abdallah akitoa neno la utangulizi kumkaribisha Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu (wapili kushoto) kuzungumza na wajumbe kwenye kikao hicho.
 Wajumbe wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Mtemvu
 Katibu Mtendaji wa Kata ya Buza, Anaclet Angelo akitambulisha watendaji wenzake kwa Mbunge
 Mzee Haombi Mwangia (kulia) na wazee wenzake wakifuatilia kwa makini katika kikao hicho ambacho wamehudhuria kama waalikwa
 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Buza Angelo akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata hiyo.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Buza Sahaibu Kapele na kulia ni Katibu wa CCM Kata hiyo, Shabani Abdallah. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...