Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, February 15, 2014

Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Hani Abdullah Mominah Akabidhi Magari 20 aina ya pick-up na Pikipiki 14 Kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
 Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa leo
 Magari 20 aina ya pick-up na Pikipiki 14 yaliyotolewa na Serikali ya watu wa Oman yakabidhiwa leo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es salaam.Vifaa hivyo vitasaidia kupunguza uhalifu katika sehemu mbalimbali nchini.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe  akiijaribu  moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo na Serikali ya Omani,  kulia Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu  Hani Abdullah Mominah  akifurahia.
Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Hani Abdullah Mominah  akizungumza jambo na Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati wa  hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo, wapili toka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe   na kulia kwake ni Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Hani Abdullah Mominah  mara baada ya makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.Picha na  Immaculate Makilika-Maelezo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...