Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 20, 2014

KASEBA NA MASHALI WASAINI MKATABA WA KUZICHAPA MACHI 29 UKUMBI WA PTA


 Mabondia Thomas Mashali (kushoto) na Japhet Kaseba wakitambulishwa na Promota wa pambano lao baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kucheza  pambano lao la ubingwa wa Mabaara wa 'Universal Boxing Organization' (UBO) pambano litakalopigwa tarehe 29 machi 2014 katika ukumbi wa Karume,  zamani ukiitwa PTA hall. 

Pambano hilo limeandaliwa na mratibu Ally Mwanzoa na zoezi la kupima afya lilifanyika jana katika ukumbi wa Vijana Kinondoni, jijini Dar es Salaam.  

Akizungumza na waandishi wa habari  kiongozi wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe aliyefatana na Anthony ruta amesema makubaliano yamekwenda vizuri na wote wametia saini kucheza pambano hilo litakalopigwa katika uzani wa kilogram 79 na wamechukua malipo yao ya awali kuashiria kuwa pambano hilo lipo na kila mmoja amejigamba kumchakaza mwenzake siku hiyo na kujitengenezea mazingira mazuri katika ubingwa wake huo.
Baadhi ya waliohudhuria zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...