Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 26, 2014

WAWILI WATANGAZWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZIL WIKI HII Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitangaza majina ya washindi wa droo ya tatu ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti mbele ya wana habari(hawapo pichani)mara baada ya kuchezesha droo mapema leo jijini Dar es Salaam, anayemshuhudia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mrisho Milao.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti wakati wa droo hiyo mapema leo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Allan Chonjo akitoa maelezo kwa wana habari mara baada ya kupatikana kwa washindi wa droo ya tatu ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti mapema leo jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Afisa Mwandamizi kutoka PWC Golder Kamuzora.
========   =======  ======

PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDEENDELEA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KATIKA DROO YA TATU.

Wawili wajishindia simu za kisasa kutoka Bia ya Serengeti.

Kwa wiki mbili zilizopita Kampuni ya Bia ya Serengeti imeweza kupata washindi kutoka mikoa mbali mbali  kama vile Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam katika promosheni yake inayoendelea nchi nzima ya WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI. Katika droo iliyochezeshwa leo kiwandani hapo washindi wawili wa ‘Samsung tablet’ walitangazwa ambako bahati hiyo iliangukia kwa Bw Mikidadi Omari (45) kutoka Mbagala, Dar es Salaam na Eddy Kisanga (67) kutoka Moshi, Kilimanjaro.

Droo hiyo iliyochezeshwa mapema leo huku ikishuhudiwa na wana habari, Maafisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, PWC na Push Mobile Media. Mbali na washindi wa droo za kila wiki kama waliopatikana leo pia kuna washindi wa bia za bure, fedha taslim na ving’amuzi kwa wiki iliyopita. Promosheni hii bado ina wiki tisa mbele za zawadi za kutosha ikiwemo ile kubwa zaidi ya safari ya Brazili.

Bw Eddy liyejawa furaha alielezea furaha yake na kutoamini kama atamiliki kifaa cha kisasa cha mawasiliano, washindi wote waliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwa na ofa kabambe kwa wateja wao kila kukicha. Eddy alisema “ninafuraha sana kuwa moja ya washindi wa promosheni hii, nilifahamu kuhusu kampeni hii kupitia vyombo vyetu vya habari vya hapa nchini na nilihamasika kushiriki. Nilisita kushiriki promosheni hii lakini  kwa ushindi huu nitaendelea kushiriki promosheni hii huenda nikabahatika tena na kupata safari ya Brazili.

Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Allan Chonjo alieleza kuwa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti inaendelea vizuri na washindi wanapatikana kutoka kote Tanzania. Allan aliongeza  “Tuna washindi kutoka sehemu mbalimbali kama Mwanza, Moshi, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam, kwetu hili ni moja ya mafanikio makubwa kufanikisha kuwafikia wateja wetu waliopo maeneo tofauti. Promosheni hii ni ya nchi nzima na si kwa wateja wa Dar es Salaam tu ila ni pamoja na wateja wetu wote hata wale waliopo mikoani.”

Washindi wa wiki iliyopita waliojipatia ving’amuzi ni Godbles Sehaba na Karushe Mathias ambao tayari wameshakabidhiwa zawadi zao na siku ya Jumamosi tunategemea kukabidhi zawadi kwa washindi wetu mkoani Mwanza Bw Jacob Nnko aliyetangazwa mshindi wa ‘Samsung tablet’ wiki iliyopita na Deus Mwikitalu aliyejishindia king’amuzi.

Kunywa kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...