Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 28, 2014

DR.MAGUFULI AKAGUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM: BARABARA YA KIMARA HADI KIVUKONI KUKAMILIKA NDANI YA MIEZI SITA


Waziri wa Ujenzi Dr.John Pombe Magufuli Kituo cha BRT kivukoni jijini Dar es salaam leo akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
 Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyekaa kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe (katikati) pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale (aliyesimama) wakisafiri kwa basi kukagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa DART Asteria Mlambo (kulia) akimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiki anayefuatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kuegesha mabasi ya haraka kinachojengwa eneo la Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari (aliyeshika kijiti) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam  

Kampuni ya Strabag International GmbH inayotekeleza ujenzi wa barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kivukoni hapa jijini Dar es Salaam imetakiwa kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa sehemu hiyo ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo kama mkataba wao unavyoelekeza. 

 Waziri wa Ujenzi Mhe. Magufuli alitoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Dar es Salaam Bus Rapid Transit - BRT) ambao umeelezewa kuwa na changamoto nyingi kiasi cha kusababisha usumbufu kwa watumia barabara hiyo kwa kipindi kirefu. 

 Akimpatia taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alimjulisha Waziri Magufuli kuwa kwa hivi sasa changamoto nyingi zimefanyiwakazi na mradi unaendelea kusimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha kuwa hukuna ucheleweshaji zaidi katika hatua hii iliyobaki.  Mkataba wa ujenzi wa barabara hizi pamoja na vituo vya mabasi ulisainiwa mwezi Desemba mwaka 2012 ukiwa umepangwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu kwa gharama ya Shilingi bilioni 280. 

 Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Saddik ambaye aliambatana na Waziri Magufuli katika ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao ndani ya sehemu ambayo mkandarasi anaendelea na kazi waondoke kwani hiyo mbali ya kuwa kinyime na taratibu za uendeshaji biashara zilizowekwa lakini pia imekuwa ni moja ya kisingizio kinachotolewa kwamba uendeshaji wa shughuli hizo unachangia kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo. 
 Waziri Magufuli akizungumza wakati wa kuhutimisha ziara hiyo, amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha mradi huo kwa muda na viwango vilivyokusudiwa. 

“Na kwa wale walio ndani ya eneo la ujenzi ni lazima sheria ichukue mkondo wake” alisisitiza Waziri Magufuli huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni Mhandisi Mussa Natty kuhakikisha anasimamia zoezi hilo la kuondoa haraka wale wote wote walioingia katika eneo hilo la barabara kinyume na sheria. 

 Aidha, Waziri Magufuli alielezea kushangazwa kwake kwa kuchelewa kuondolewa kwa nyaya za Tanesco katika maeneo ya City Squire na Morocco kwani fedha za kutekeleza kazi hiyo tayari zimelipwa muda kirefu. 
“Ucheleweshaji wa ainaa hii ndiyo unaotoa mwanya kwa mkandarasi kuanza kutoa visingizio vya kutokamilika kazi hii kwa wakati” ametahadharisha Mhe. Magufuli. 

 Hata hivyo katika hatua nyingine Mhe. Magufuli amemtaka mkandarasi kuharakisha taratibu za kuifungua barabara hiyo upande wa kuingia Dar es Salaam ambako kwa sasa hivi hakuna shughuli kubwa zinazofanyika ili kupungiuza adha ya msongamano wa magari yanayopishana katika njia moja ya upande wa kutokea mjini katika barabara hiyo ya Morogoro hasa kwa eneo kati ya Ubungo na Kiamara. 

 Naye Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS Mhandisi Barakaeli Mmari ameelezea kuwa, utekelezaji wa mradi huu wa usafiri wa haraka utajengwa katika awamu sita.  Awamu ya kwanza ambayo ujenzi wake ndio huu unaoendelea inahusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni – Morocco na Faya – Karikaoo. Hadi sasa mkandarasi amekwisha kamilisha asilimia 55 ya mradi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...