Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 24, 2014

Washindi wawili wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti wakabidhiwa zawadi zao


  mshindi wa king’amuzi cha azam katika promosheni ya winda safari ya Brazili na Serengeti Bw Godbles Sehaba katikati akikabidhiwa zawadi yake  na meneja mauzo eneo la mabibo Bi Anna Gassembe (kushoto) na afisa mauzo Bi Anna Msonga (kulia).
Washindi wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti Godbles Sehaba (kulia)na  Karushe Mathias  (kushoto) wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa zawadi zao za king’amuzi cha azam walizoshinda baada ya kuchezeshwa droo hiyo siku ya jumatano.

Washindi wawili wa droo ya winda safari ya Brazili na Serengeti wamekabidhiwa zawadi zao jumamosi katika bar ya muleba iliyopo maeneo ya Mabibo Dar es Salaam, washindi hao Bw Godbles Sehaba na Karushe Mathias wakiwa na furaha walipokea zawadi hizo na kuishukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwapa zawadi hiyo, wakiwa kama mashabiki wakubwa wa soka la nyumbani washindi hao wamefurahia kupata zawadi itakayowawezesha kuangalia ligi za mpira wa miguu ya nyumbani bila matatizo.


Meneja mauzo eneo la mabibo hilo Bi Anna Gassembe ambaye alikabidhi zawadi kwa washindi amehimiza watu kuendelea kunya bia ya Serengeti kistaarabu ili wajishindie zawadi. "zawadi bado ni nyingi na zawadi kubwa ya safari ya Serengeti bado haijatolewa kwa hiyo muendelee kushiriki zaidi ili mjipatie zawadi mbalimbali" alisema Anna.promosheni ya winda safari ya Brazili na Serengeti inaendelea na washindi wanaweza kujishindia zawadi za simu aina ya samsung galaxy tab, king'amuzi cha azam, pesa taslimu shilingi 5000 na 10000, bia za bure pamoja na zawadi kubwa ya safri ya kwenda Brazili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...