Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 10, 2014

HATIMAYE MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KWA AJILI YA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA YATANGAZWA RASMI.Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) , Sharon Mariwa  Meneja wa Mahusiano OXFAM, Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB pamoja na Mkamiti Mgawe Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM, wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa katika Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula leo.
Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akielezea Mchakato mzima wa kazi ilivyokuwa kabla , wakati wa kuwatafuta washiriki wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula na kutaja rasmi majina ya waliochaguliwa katika usahili huo.

   Meneja wa Mahusiano OXFAM Sharon Mariwa  akielezea utaratibu utakao fuatia baada ya kutangazwa rasmi majina ya waliochaguliwa katika shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula
 Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB akitilia mkazo baadhi ya mambo wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa kuingia Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
 Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Kipanya) akijibu Maswali yaliyo ulizwa na waandishi wa Habari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...