Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 24, 2014

MADAKTARI INDIA: MTOTO ALICHELEWESHWA
Hamis Hashim Liguya akiwa katika Hospitali ya Ganga,mjini Mombai India.

SIKU chache baada mtoto Hamis Hashim Liguya (13) aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu kuwasili nchini India, jopo la madaktari mjini Mombai, limesema mtoto huyo alicheleshwa kupewa matibabu kwani angewezekana kutibiwa mapema.


Jopo la madaktari wakiongea jambo.

Mtoto huyo aliwasili Uwanja wa Kimataifa wa Coimbatore hivi karibuni na haraka madaktari wa Hospitali ya Ganga, India walimpokea na kuanza kumpima vipimo vya awali kabla ya kumfanyia upasuaji.

Kila daktari katika jopo hilo, alimchukua kipimo chake kisha mwishoni waliutaja ugonjwa unaomsumbua mtoto huyo unaitwa tuma na umemshambulia hadi kwenye uti wa mgongo lakini kama ungewahishiwa tiba mapema Tanzania, isingefikia hatua iliyopo ambayo wanadai uwezekano wa kutembea ni mdogo hata akapofanyiwa upasuaji.


Madaktari wakikagua X- ray.


“Hili tatizo lingeweza kuwahiwa lisingeweza kufikia hatua hii, wamemchelewesha kumpatia matibabu, wangemwahisha mapema na kumpa tiba sahihi, tatizo lisingefikia hatua hii,” alisema mmoja wa madaktari ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.


Mtoto huyo ambaye ameteseka kwa muda mrefu na ugonjwa huo na madaktari wa Tanzania kushauri apelekwe India, aliondoka nchini Jumamosi iliyopita akiwa ameambatana na baba yake mzazi, Hamis Mwiguya na mwandishi wa Global Publishers, Imelda Mtema. Kampuni ya Global Publishers Ltd inayozalisha magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, ndiyo ilikuwa ya kwanza kuripoti habari za ugonjwa wa mtoto huyo, kisha wakajitokeza wadau na wananchi wengine kumsaidia fedha ambazo zilimwezesha kwenda nchini India kutibiwa.
Miongoni mwa wadau ambao walijitokeza kutoa msaada wa kumtangaza, ni mtangazaji Hoyce Temu wa kipindi cha Mimi na Tanzania aliyejitoa kumsaidia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...